Siku ya wapendanao ni sikukuu ambayo
huadhimishwa ifikapo Februari 14 kila mwaka. Historia yake imeanzia karne ya
tatu nchini Italia.
Kuna wanaume na wanawake, leo ni sherehe yao
ya kufanya ngono/uzinzi, wakifikiri kwamba ndiyo maana ya siku hii ya Valentine
Day, kitu ambacho si kweli. Usahihi ni kwamba siku hii imelenga kuhamasisha watu
kupendana, ndiyo kusema kwamba unaweza kuonyesha upendo kwa mtu yeyote, si
lazima awe mwenza wako.
Tujaribu kufikiria hasa nani anahitaji upendo kuuadhimisha siku ya leo? Je ni yule alionao au yule aliokukosa kwa muda mrefu?
Mimi ninavyoona Watu tungetumia siku ya leo kuonesha faraja kwa wale waliokosa faraja, kwa mfano kuwatembelea watoto yatima, kuwasaidia wazee wasiojiweza, kutatua matatizo japo kidogo kwa wale wanaohitaji kama wafungwa, wagonjwa, Yatima, na watoto wamitaani.
Love clinic leo imeona ikuletee wazo hili kama ukiona ni la msingi basi ungana na Love Clinic kuweza kuhitimisha siku hii kwa mambo haya.

Nchini Italia wakati huo kulikuwa na kiongozi aliyeitwa Mfalme Claudius II; aliamini kuwa askari anapooa hawi mkakamavu na pia muda mwingi anawaza kuhusu familia yake zaidi ya kitu kingine chochote.
Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa
askari. Kitendo hicho hakikuwafurahisha watu wengi, akiwamo Padri Valentino.
Kiongozi huyu wa kidini aliendelea kufungisha ndoa kwa siri. Mfalme Claudius
alipopata habari hizi aliamuru Valentino akamatwe na kuuawa. Mtakatifu
Valentino aliuawa siku na tarehe kama ya leo, ndiyo maana ikatangazwa rasmi
kuadhimishwa kwa ajili ya kumkumbuka kama Baba wa Upendo na mtetezi wa
wanandoa.


Historia zinaonyesha kuwa
aliyetangaza rasmi kuadhimisha siku hiyo ni Papa Gelasius. Aidha, iko simulizi
nyingine inayosema kuwa akiwa gerezani Valentino aliandika barua ambayo ilikuwa
na salamu za Valentino kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua
alihitimisha kwa kusema ‘Kutoka kwa Valentino wako’. Tangu hapo Valentino
anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa ulimwenguni
kote.
Siku hii inaonekana ni maalumu
kwa ajili ya kuonyeshana upendo wa dhati kwa mtu yeyote. Ni siku muhimu na yenye
maana kubwa kwa kila mtu, maana upendo hauchagui. Ingawa wengine wanaweza
kuitumia au kuichukulia kwa kadri wanavyotaka, msingi wa siku hii hasa ni
kuonyesha upendo kwa watu, si lazima awe mke au mumeo ama mchumba.
Maana na ukweli wa uwepo wa siku
hii inayoitwa Valentine’s Day inaharibiwa na baadhi ya watu kwa kuiona kama ni
siku ya kufanya ngono/uzinzi. Ukitaka kuthibitisha hili, siyo lazima uende chuo
kikuu ili kupata ujuzi wa kujua ukweli, bali tembelea nyumba za wageni zilizo
karibu, nyingi utakutana na bango ‘vyumba vimejaa!’
ZAIDI KUHUSU SIKU HII
Siku hii inaonekana ni maalumu
kwa ajili ya kuonyeshana upendo wa dhati kwa mtu yeyote. Ni
siku muhimu na yenye maana kubwa
kwa kila mtu, maana upendo hauchagui.
Ingawa wengine wanaweza kuitumia
au kuichukulia kwa kadri wanavyotaka, msingi wa siku hii
hasa ni kuonyesha upendo kwa
watu, si lazima awe mke au mumeo ama mchumba.
Maana na ukweli wa uwepo wa siku
hii inayoitwa Valentine’s Day inaharibiwa na baadhi ya watu
kwa kuiona kama ni siku ya
kufanya ngono/uzinzi. Ukitaka kuthibitisha hili, siyo lazima uende
chuo kikuu ili kupata ujuzi wa
kujua ukweli, bali tembelea nyumba za wageni zilizo karibu, nyingi
NAMNA INAVYOPASWA
Msingi hasa wa siku hii ni
kuonyesha upendo, hii ina maana kuwa unaweza kuonyesha upendo
kwa yeyote iwe ni jirani, mzazi
au yeyote unayempenda, siyo lazima mpenzi kama ambavyo baadhi ya watu
wanafanya.
Waweza kumtumia ujumbe mzuri mtu
yeyote unayempenda au hata zawadi, waweza kutembelea yatima, wagonjwa na hata
watu wengine wowote; kubwa hasa kwa siku hii ni kuonyesha upendo. Hata hivyo,
kwa sababu ya ukweli kwamba wengi wanaiona kama ni siku ya ngono, ni suala la
msingi sana unapotoa zawadi kwa mtu wa jinsi tofauti kuwa makini; angalia
zawadi unayoitoa isije ikaharibu siku yako na maisha yako kwa jumla badala ya
kukupa furaha, kwa sababu baadhi ya wenza wa wale ambao unaweza kuwapa zawadi
wanaweza kutafsiri kama wewe una uhusiano wa kimapenzi na mtu huyo.


Wataalamu mbalimbali wa masuala
ya uhusiano, wanasema katika siku kama hii ya leo, ni vizuri walio kwenye
uhusiano mbaya kujifunza namna ya kuwa na uhusiano mzuri, kwani ubaya hauna
maana katika maisha. “Hii ni siku muhimu kwa kila mtu kuangalia uhusiano wake
na watu wanaomzunguka,” anasema Hi Song, ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya
Uhusiano nchini Marekani kutoka Kituo cha Ushauri cha Marriage Life. Anasema
kuna ambao huanzisha uhusiano siku hiyo kwa lengo la kupata mtu wa kustarehe
naye, hili ni kosa. Kama mtazamo wako ni kutafuta mpenzi m
ONDOA MAWAZO MABAYA
Ondoa fikra mbaya kichwani mwako.
Waza kuhusu mema na kupendana kwa dhati, hapo utakuwa umekwenda sawa na maana
ya siku hii. Kuna watoto wanaoishi katika mazingira magumu, wazee na wahitaji
wengine. Tumia ulichojaliwa kushiriki nao katika siku hii ya leo, badala ya
kuwaza ngono au uzinzi. Siyo lazima iwe fedha, hata chakula na mavazi.
Inawezekana una nguo unazodhani hazifai, wape wenzako ambao wanahitaji hapo
utakuwa umeonyesha namna unavyotambua na kuiadhimisha kwa usahihi
Endelea kuitembelea Love Clinic
kwa kuisapoti kuiporomoti, tupia comments zako hapo chini tuende pamoja
Kwa lolote la kujenga na
kuimarisha mahusiano usisite
Email: mossesshio@gmail.com
Mobile: +255745222780
0 comments :
Post a Comment