Karibu Love Clinic Leo Tujifunze......
Kila mahusiano yanachangamoto zake na maana halisi ya mahusiano ni yale yenye uwezo wa wanamahusiano hao kuvumiliana katika
changamoto mbali mbali. Kuna changamoto za kimungu ambazo wanandoa hawawezi kuziepuka
lakini kuna zile za kiuanadamu ambazo nyingi ni za kimakusudi na mtu huamua tu
kuwa hivyo. Katika kuangalia ndoa leo nimeona nichambue aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka kuwa nao;
(1) Wanaojione Kama Wafalume (King Husband); Hii ni
aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake
zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni
kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka
waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke
hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini,
wote kimya hakuna hata kuongea.
(2) Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband); Hii
ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo
kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya
mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila
kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama
ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi
ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.
(3) Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband); Hawa
hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya msingi, mambo hayaishi, kosa la
mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na
mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa
nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke.
(4) Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband); Hawa
wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa
mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema
hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa
hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata
wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.
(5) Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband); Hawa
wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa
ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata
hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na
wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua
maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao.
(6) Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol
Husband); Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na
wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke,
wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata
kuleta vizawadi, wanajua udhaifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia
mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali
tena.
(7) Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband); Bado
wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa
ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na
kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa
na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani
alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi
kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya
ndoa.
(8) Mume Mtalii (Visiting Husband); Hawa
wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu
lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na
hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na
marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na
mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata
atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto.
(9) Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband); Hii
ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke
anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na
alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni
wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni
mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi
hampi pumzi mwanamke.
(10) Mwanaume Mbahili (Miserly Husband); Huyu
anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia
matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari
ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela
labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke
akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine
kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.
Hizo nji baadhi tu ya aina ya wanaume ambao
wanawake wengi wasingependa kuwa nao. Kama mwanaume upo hivyo jua mke wako
hafurahii na anavumilia tu. Ndoa ni furaha amua kubadilika na usimfanye mke
wako kuishi na wewe kwa kujilazimisha. Kama ni mume jiulize uko namba ngapi
hapo
Jifunze Zaidi na kupitia LoveClinic
Tunakukumbusha tu kama una changamoto yeyote au tukilo
linalohusiana nasi usisite kuwasiliana nasiku kwa:
Email: mossesshio@gmail.com
Mobile: +255 (0) 745 222 780
0 comments :
Post a Comment