JE? NI SAHIHI MPENZI WAKO KUENDELEA KUWASILIANA NA X WAKE? TOA MAONI YAKO HAPO CHINI...





Hayo ndiyo mapenzi jamani! Tumekua tukisikia na kuona hata kwa ndugu jamaa na marafiki namna wapenzi wanavyo lalamika kwa watu walio karibu nao.

Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume anaweza kujikuta unaangukia kwa msichana ambaye tayari ameshatoka kuumizwa pasipo rasmi ya kuachana na ndipo pia msichana kujikuta akiingia kirahisi kwa kufikiri kutuliza maumivu ya wakati huo pasipo kujipa muda kwa kisingizio cha kua na stress.

Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?


Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mahusiano na msichana mwingine walioukua wamehskua mbali lakini pande moja inavuta kurudi walikokua mwanzo hapo unakuja kugundua kua kumbe ulipoingia nay eye ana mtu wake. Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako pamoja na kukupa fursa ya kua wewe ndio chaguo lake.

LOVE CLINIC INAKUPA MAMBO KADHAA ( KWA UCHACHE ) YA KUKUSAIDIA KUKABILIANA NA HALI HII.


Chunguza
Unapojikuta umeingia katika mahusiano mapya usijikite moja kwa moja kwa siku moja au wiki kujiona umefika mahali ulipotegemea cha kwanza tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake wa awali kama ulishakoma au bado kuna chembe chembe za mawasiliano na ni kwa muda gani.

Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye nay eye asilitambue hilo. Ndiyo maana nikasema chunguza uhusiano wake kwanza.



Usitafute uadui
Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaendelea na mawasiliano ya maara kwa mara kwa kupigiana simu kuchati au hata kuonana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.


Una nafasi kwake?
Sawa umetokea kumpenda msichana/mvulana aliye mpya kwako, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.


Ni rahisi kubadili uamuzi wake?
Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kuacha mambo unayoweza kuyaona hayafai mbele ya uhusiano wenu mambo yanayoweza kuhatarisha uhusiano wenu kuyumba, kama kweli hana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.


Pingana na moyo wako
Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na msichana au mvulana ambaye tayari ana ameachana au anampenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.
Kwa hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha kumng’ang’ania msichana/mwanaume mwenye mpenzi wake licha ya ukweli kwamba, huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya kuwa mume/mke wake na siyo huyo aliye naye.


Urafiki ni sawa?
Umempenda sana na hauko tayari kumkosa katika maisha yako lakini imetokea kwamba tayari yuko na mtu na umebaini huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba angalau urafiki. Siyo urafiki wa kivile sana ila angalau pale unapotaka kusikia sauti yake kwa kumsalimia tu, upate nafasi hiyo.


Usiumie, yupo mwingine
Haina haja ya kujitafutia vidonda vya tumbo bure wala kujipa stress kwenye maisha yako kwa kuwa tu umebaini uliyetokea kumpenda tayari ana mtu. Chukulia ni hali ya kawaida, wakati mwingine moyo husukuma sana na kuumia kwa kujiona umenyanyaswa lakini si jambo la kuweka sana katika moyo na akili yako cha msingi ni kufocus na kutazama mbele. Wanaume na wasichana wazuri ambao wanaishi singo wapo kibao huko mtaani, ni suala la wewe kutulia tu. Amini yupo mwingine ambaye atayafanya maisha yako yawe ya furaha.


Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana kuhakikisha unampata kwa sababu ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa gizani. Ila pale utakapoona uwezekano wa kuwa naye haupo, usilazimishe ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha tu!

Love Clinic inakukaribisha sana kutembelea blog hii kila mara ili uweze kuelimika Zaidi kila siku na kujifunza changamoto mbali mbali ili nawe uweze kuzishinda.

Tunakushauri kama unajambo lolote, swali, changamoto, maoni na ushauri, ama tukio lolote ilimradi liwe la kweli tunakukaribisha katika safu ya ukurasa wetu.

Wasiliana nasi kwa:
Whatsapp: +255745222780


Share on Google Plus

About Mlaki

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment