Kila mwanamke ana sifa zinzomtosheleza yeye mwenyewe kwa jinsi alivyoumbwa lakini sifa tunazozungumzia hapa ni zile sifa bora ambazo wanawake wote wameumbwa nazo isipokua hawazitekelezi kama ambavyo wanatakiwa kutekeleza sifa hizo. sasa basi leo tujifunze mwanamke bora ni mwenye sifa zipi?
Sifuatazo hapa chini nimekuletea sifa za mwanamke anazostahili kua nazo katika maisha yake hasa kwenye maisha ya mahusiano kama unavyojua hii ndio shughuli yetu Kubwa hapa Love Clinic kukuletea mafunzo imara na yanayokufundisha zaidi ya unachokifahamu.
Wenye msimamo
Wanawake
daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa
mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na
siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
Wenye Kupenda
usawa
Aina ya pili
inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu
usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa
na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.
Wanaojua
mapenzi
Wanawake
wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa
kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu
katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka
akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.
Marafiki
Wanawake
wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea
zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na
kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa
wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.
Wa wazi
Aina
nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi
wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake.
Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye
tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.
Wanaoweza
kujitegemea
Wanawake
wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha
kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake
tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.
Wasio na
presha
Nikisema
wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka
haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu
ya majukumu yao kama wapenzi.
Maridadi
Kundi
lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na
kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni
welewa wa mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa muonekano.
Wanaoridhika
Wanawake
ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni
kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume
ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu.
Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.
Wa mmoja
Wanawake wanaochagua mara
moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa
wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika
sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la
wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
0 comments :
Post a Comment