Kwa mwanamke kumpata mwanaume
mwenye muafaka, yaani mwanaume ambaye ni husband material si kazi rahisi.
Inaweza kuchukua miezi kama siyo miaka ya kucheza pata potea kabla ya kumpata
mwanaume halisi wa ndoto yako. hata hivyo wakati mwingine inaweza kutokea mwanamke
akafanya majaribio kadhaa ya kuwa na mitoko (dating) na wanaume tofauti tofauti
na bado akajikuta anatoka kapa, yaani hakuna hata mmoja anayefikia viwango
vyake alivyojiwekea na kujikuta umri unasonga na bado wako single. Jambo hilo
huwachanganya sana wanawake wengi na kuwaletea msongo wa mawazo au vurugu
kichwani na kuonekana kama vile wamedata wakati siyo kweli ni kutokana na
mapito katika harakati za kumpata mwenza mwenye muafaka.
Hapa chini nitaeleza sababu
zinazosababisha wanawake wengi kukwama pale wanapokuwa kwenye harakati za
kutafuta mwanaume wa ndoto zao:
1. Hujui unatafuta mwanaume wa
aina gani?
Huu ni ujinga unaofanywa na
wanawake wengi. Kuna idadi ya kutosha ya wanawake ambao wanakuwa na mitoko na
wanaume wa aina tofauti tofauti lakini ndani ya nafsi zao hawajui wanataka
kuolewa na mwanaume wa aina gani. Mbaya zaidi wanawake hawa wanajikuta
wakipoteza muda wao mwingi wa kuwa na mitoko lakini hawajui wabnachokitafuta,
mwisho wa siku hujikuta akiwa ametoka na wanaume wengi sana lakini hakuna hata
mmoja waliyemuona anafaa, na jambo hilo huwa linawachanganya na kujikuta wakiwa
na msongo wa mawazo, kumbe masikini ya Mungu hawajui kwamba mwanaume
wanayemtafuta anafananaje.
2. Kujihisi kutokuwa salama
Kama mwanamke anajihisi kutokuwa
salama anapokuwa na mtoko kunamuweka katika mazingira ya kutompata mwanaume
anayemtarajia kwa sababu hana uhakika anatafuta mwanaume wa aina gani.
Kutojiamini kwa mwanamke kunamfanya kushindwa kufanya juhudi binafsi za kumnasa
mwanaume wa ndoto zake kutokana na kujiuliza maswali mengi kwamba mwanaume
aliye mbele yake ndiye au siye? Mwanamke kutokuwa na uhakika kama atataka
mwanaume wa aina gani kunamuweka katika mazingira ya kushindwa kumvutia
mwanaume mwenye muafaka hata kama aakuwa na mtoko naye mara kadhaa. Kumbuka tu
kwamba maamuzi ya kuwa na uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke yapo zaidi kwa
mwanamume, hivyo ili mwanaume aweze kujenga uhusiano na mwanamke ni lazima
mwanamke huyo amvutia. Kwa kitendo cha kutojiamini mbele ya mwanaume kinamuweka
mwanamke katika mazingira ya kuwekwa pembeni. Ni pale tu utakapokuwa umejua
unachokitaka au aina ya mwanaume unayemtaka ndipo utakapojiweka kwenye nafasi
nzuri ya kutengeneza nafasi ya kukutana na wanaume wa aina hiyo na ukichanganya
na kujiamini ndipo utakapofanikiwa kumvutia mwanaume huyo na kumnasa.
3. Ukosefu wa mbinu za kuwanasa
wanaume wenye muafaka
Kwa kawaida kila mtu ana udhaifu
wake, hivyo linapokuja suala la mtoko, kila mmoja anajaribu kuwa makini kuficha
udhaifu wake. Ukweli ni kwamba jambo hilo linaweza kuwa ni kikwazo kwa mwanamke
kumpata mwenza sahihi. Unakuna mwanamke anakuwa na mtoko na mwanaume na katika
mazungumzo tu ya kawaida anajitahidi sana kutotofautiana na mwanaume aliyetoka
naye au anajifanya ni malaika asiyekosea na kujitahidi kuonyesha rangi yake
halisi kwamba yeye ni mwanamke wa aina gani. Ni nyema mwanamke akajipambanua na
kuonyesha kwamba yeye ni mwanamke wa aina gani kwani yaweza kuwa kwa jinsi yeye
alivyo na anavyoyachukulia mambo ikawa ni sifa ambayo inaweza kumvutia mwanaume
aliyetoka naye....
4. Mwanamke anaweka nguvu nyingi
kwa aina moja ya mwanaume anayemtarajia
Katika mchakato wa kuwa na
mitoko, mwanamke anakuwa amejiwekea aina moja ya mwanaume anayemtaka na
anaelekeza nguvu nyingi katika kumtafuta mwanaume wa aina hiyo hiyo. Si vibaya
kujiwekea malengo na matarajio kwa aina ya mwanaume unayemtaka lakini vigezo
vyako vinakufungwa kwa aina moja tu ya mwanaume hilo ni tatizo. Jaribu kutoka
kidogo nje ya vigez ulivyojiwekea inaweza kukusaidi kujua aina tofauti tofauti za
wanaume...
5. Bado unatembea na kumbukumbu
ya mwanaume/wanaume ulioachana nao
Kwa kawaida wakati mwingine ni
ngumu sana kuendelea na maisha yako ya kawaida baada ya kuachana na mpenzi wako
uliyempenda sana, hasa kama mlikuwa pamoja kwa kipindi kirefu kidogo na
mlipendana sana. Hata hivyo kama bado moyo wako umekuwa ni mgumu kumsahau
mpenzi wako mliyeachana itakuwa ni vigumu kuwa na mitoko na kumpata mwanaume wa
ndoto zako. kwa kifupi ni kwamba hutofanikiwa kwa sababu hujakuwa tayari.
6. Unajitahidi sana kuchukua
tahadhari kupita kiasi....
Baada ya kuwa mwanamke ameumizwa
sana katika mahusiano yake ya nyuma mara nyingi humuwia vigumu kusahau na
kusonga mbele. Lakini pia huyachukulia mahusiano kwa tahadhari kubwa. Kwa
kawaida si ajabu kukuta mwanamke aliyetendwa akiwa amejiwekea ulinzi madhubuti
dhidi ya wanaume akijitahidi kwa kadiri awezavyo kuwakwepa na hata kuwakataa au
kuwakatisha tamaa kwa kuogopa kuumizwa tena. Lakini ukweli ni kwamba kamwe
haiwezekani mwanamke kupata mwenza wa ndoto zake iwapo hatakuwa na moyo wa
kuthubutu hata kama atakuwa ameumizwa katika mahusiano yake ya nyuma, mara
nyingi tunashauriwa kuyatumia makosa yetu kama elimu ya kutuwezesha kufikia
matarajio yetu, kwa kuumizwa mara kadhaa kunampa mwanamke uwanja mpana wa
kuwajua wanaume wakware na hila zao. hata hivyo inashauriwa mwanamke kujipa
muda kidogo ili kuponya kidonda cha kuumizwa katika uhusiano kabla ya kuanza
kuwa na mitoko na wanaume wengine watakaoonekana kuvutiwa naye, kwani kama
akiharakisha anaweza kushindwa kumshawishi mwanaume aliyetoka naye kutokana na
kutojiamini.
7. Kazi inachukua sehemu kubwa ya
maisha yako...
Mtu kuipenda kazi yake siyo kitu
kibaya, lakini si vyema kazi yako ikachukua sehemu kubwa ya maisha yako na muda
wako kiasi cha kukufanya ushindwe kujichanganya katika mambo ya kijamii au kuwa
na mitoko itakayokukutanisha na watu mbalimbali wa kubadilishana nao uzoefu.
Wakati mwingine mwanamke anaweza akajikuta hapati mwanaume wa kumuomba mtoko
kwa sababu ya kuonekana kwake kuwa na udhati (serious)na mambo yake au kazi
yake. Unaweza kumkuta mwanamke muda wote yuko bize na kazi kiasi cha kukosa
muda wa kuchangamana na watu wengine. Mwanamke wa aina hii ni vigumu sana
kupata mwanaume wa ndoto zake. Inashauriwa ili kumpata mwanaume wa ndoto zake
ni vyema mwanamke akajiunga na vikundi vya kijamii hususan kwa huku kwetu viko
vikundi kama Vikoba vinavyowakutanisha watu mbalimbali kwa shughuli za kiuchumi
au kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ambazo ni rahisi kuwakutanisha
watu.
8. Kuwa na mtazamo hasi
(Negative) kuhusu wanaume
Huwezi kamwe kumpata mwanaume wa
ndoto zako kama una mtazamo hasi kuhusu wanaume. Kama unatawaliwa na fikra za
kukata tamaa au kuna sauti ndani yako (little Voices) zinakwambia kamwe huwezi
kumpata mwanaume sahihi kwa sababu wanaume wa kuoa wamekwisha au hawapo, na
ukaamini na kujenga hofu, ni dhahiri kwamba haitatokea kumpata mwanaume sahihi
kama ulivyoamini. Kumbuka kwamba sisi ni kile tunachowaza na kuamini kwa hiyo
ni kiasi tu cha kubadilisha mawimbi yako ya namna ya kufikiri kwa kuwaza mambo
mazuri unayoyahitaji huku ukiamini kabisa kwamba inawezekana. Lakini pia labda
nitoe ushauri wa bure kwa wanawake. Kama unataka mwanaume wa ndoto zako awe wa
namna gani basi tengeneza picha yake kichwani mwako na kisha kila siku asubuhi
fanya tahajudi kwa dakika kumi tu, na nuia kwamba ungependa ukutane na mwanaume
huyo na akupende mfunge ndoa na kuzaa watoto.
9. Kila mwanaume anayekuomba
mtoko unagundua siyo sahihi kwako
Kuwavuta wanaume wasiyo sahihi na
wasiokidhi viwango vyako kunachangiwa na mambo mengi. Hebu chunguza mawazo
yako, chunguza marafiki zako unaoambatana nao, chunguza maeneo unayoishi,
chunguza maeneno unayotembelea, Je wewe ni mwanamke wa aina gani, una tabia
gani nk......... Ni vyema kama unajiwekea malengo ya kumpata mwanaume mwenye
tabia uzitakazo, basi mchakato wa kumpata ni pamoja na kujiweka katika
mazingira ya kumvutia mwnaume huyo. Isije ikawa unatamani kumpata mwanaume
msomi mcha Mungu na mchapa kazi na anayejali familia (sifa ambazo wanawake
wengi huzitamani) lakini wewe mwenyewe hauko hivyo, sasa utatengenezaje
connection ya kukutana na mwanaume huyo! Kumbuka pia mwanaume wenye haiba hiyo
naye ana ndoto zake ni pale tu ndoto zenu zitakapo match ndipo makapovutana na
kukutana na kufikia kufunga ndoa na kujenga familia bora.
10. Unawalinganisha wanaume
kupita kiasi
Ni vyema kujifunza kutokana na
makosa uliyowahi kuyafanya katika mahusiano yako ya nyuma, lakini makosa hayo
yasigeuke na kuathiri mtazamo wako kuhusu wanaume. Ninachotaka kusema hapa ni
kwamba si vyema kumlinganisha kila mwanaume unayekutana naye na mwanaume
uliyewahi kuwa na uhusiano naye huko nyuma. Kila unapokuwa na mtoko na mwanaume
nenda huku kichwa chako kikiwa kitupu kabisa ili kupata mtazamo mpya kuhusu
mwanaume huyo kutokana na mazungumzo yenu. ukiwa tayari una hofu za kujiuliza
kama atakuwa ni mwanaume sahihi au atakuwa kama fulani, ni kama vile
umeshamhukumu na kila jambo atakalofanya au kusema utakuwa na mjadala mzito
kichwani ukijaribu kulinganisha na kutafuta majibu jambo ambalo litakufanya
usiwe na uzingativu kwenye mazungumzo yenu.
Kwa sababu hizo hapo juu Je wewe kama mdau wa Love Clinic Unaemaje na unalipi la kuongezea au kutupa uwazi kwa jambo hilii na nini kifanuyike ili kuweza kuwapa urahisi ndugu zetu hawa
usisite kutembelea blog hii ya LOVE CLINIC ili uendelee kuelemika na kujifunza mengi.
kama una maswali, shuguda., hadithi au changamoto ama tukio lolote wasiliana nasi kwa mawasiliano haya hapa chini
Email: mossesshio@gmail.com
Whatsapp: 0745222780
0 comments :
Post a Comment