AFYA: ZIJUE AINA 10 ZA VYAKULA UNAVYOPASWA KULA WAKATI UNAPOKUWA KWENYE SIKU ZAKO (PERIOD)

Huu ndio ushauri wa kiafya unaotolewa na madactari wetu wanaoshirikiana nasi hapa Love Clinic katika kuboresha afya za wanafamilia wa Love Clinic.


Swali Ni Je wazijua aina za vyakula ambavyo watakiwa kula wakati wa Siku zako za hedhi (Period)
Katika kipindi cha mzunguko (siku za hedhi) kwa kawaida wanawake hupoteza kiasi cha damu pamoja na baadhi ya madini mwilini.

Hali hiyo huweza kusababisha upungufu wa damu kama mwanamke atakuwa hapati lishe bora na ya kutosha. Sasa ili kuzuia upungufu wa damu na madini mwilini, msichana/mwanamke anatakiwa kula vyakula vyenye madini chuma na chokaa kwa wingi ikiwa ni pamoja na hivi vifuatavyo:-

Orodha ya vyakula vinavyopendekezwa

1. Mboga za majani
2. Maharage
3. Soya
4. Samaki
5. Maziwa
6. Korosho
7. Mayai
8. Zabibu (Juisi yake)
9. Matunda damu
10. Dagaa n.k.

Pia zipo aina za matunda /Juice ambazo pia hutibu au kupunguza maumivu wakati wa hedhi kwa mwanamke kwa kiasi kukikybwa ambazo ni hizi zifuatazo:

1. Ndizi Mbivu
2. Papai
3. Tangawizi nazo hutibu kwa kiasi kikubwa.

Mbali na vyakula hivyo, pia mwanamke huhitaji kunywa maji ya kutosha kipindi hiki na kuzingatia hali ya usafi wa mwili, hasa sehemu za siri. Tumia vitambaa safi vilivyo nyooshwa kwa pasi au pedi zilizohifadhiwa katika hali ya usafi.

Una maoni yeyote swali au ushauri  wasiliana nasi kwa simu namba +255 745 222 780, +255 713 222 705 au barua pepe mossesshio@gmail.com.


Share on Google Plus

About Mlaki

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment