UNAZIJUA AINA ZA WANAUME WANAOPENDWA ZAIDI NA WANAWAKE


LOVE CLINIC iko kwa ajili yako na kukujuza mengi katika kuyatambua mahusiano na maisha ya kila siku Kuna wakati nilijaribu kuwauliza wanawake kadhaa walioolewa kama wamefanikiwa katika ndoa kupata aina ya wanaume waliokuwa wametarajia. Wengi walikuwa wanasita kunipatia jibu la moja kwa moja kama ndiyo au hapana.



Lakini nilipowauliza kama kuna tofauti kati ya hisia za wanaume wa zamani kwa wanawake na za wanaume wa leo zaidi ya nusu walikiri kuwa kuna mabadiliko chanya.

Kila ninapoandika kuhusu mahusiano katika mahusiano au ndoa kati ya mume na mke nakuja kugundua kua Wanaume wengi siku hizi wanapowafikiria wenzi wao katika ndoa wanahoji usahihi wa fikra walizokuwa nazo mababu zetu kuhusu hadhi ya mwanamke katika jamii na falsafa iliyotumika katika kumuenzi zaidi mtoto wa kiume na kumuweka nyuma wa kike.

Siku moja nilipokuwa nikisikiliza mazungumzo ya wanaume wanaotoka kwenye makabila yaliyokuwa yakiongoza katika mila za kuwaweka wanawake nyuma, niliamini kuwa sasa wanaume wamebadilika. Walisema:

“Sisi wanaume wa siku hizi tunakabiliwa na shinikizo la hoja za usawa wa kijinsia ambalo ingawa linapingana na mila zetu hatuna budi kupima kama zina mashiko katika maisha ya sasa ambayo ni tofauti sana na yale ya zamani.”

Mwanamke wa leo anawajibika kujijengea siyo tu uwezo wa kuilea familia yake, bali pia kujenga haiba na hadhi yake katika jamii na kupanda ngazi za juu katika kazi yake na pengine hata juu kuliko wanaume.

Mwanamume akumbuke kuwa licha ya kumsaidia mkewe katika shughuli za familia, yeye ndiye mwenye jukumu la kumsaidia kufanikisha ndoto zake za kutukuka katika jamii na katika kazi yake. Wanawake wamekuwa wakitekeleza jukumu hili kwa waume zao kwa miaka mingi. Hata kuna methali ya kiingereza isemayo “The road to success if full of women pushing their husbands in wheelbarrows” Yaani njia ya kuelekea kwenye ufanisi imejaa wanawake wanaowasukuma waume zao katika matoroli.”



Wanaume wa kisasa, kama alivyo Obama wamejifunza kuwa mwanamke wa leo sio tena yule wa zamani ambaye alifikiriwa kama mama wa nyumbani tu asiye na mchango wowote katika maendeleo ya ulimwengu huu yanayokwenda kwa mwendo wa kasi hata kuliko sasa.

Wanawake wa sasa wanapenda mwanaume anaejua kushughulika katia maeneo mengi ya kutafuta maisha, mwanaume anaejua kujali na kuthamini, mwanaume asie kua muongo (mkweli wa mambo yake) na asie na kupinda pinda, mwanaume mtanashati na asiependa ujana sana hasa katika mavazi muonekano kwa ujumla pamoja kusikiliza katika majadiliano

Aidha, ninapokaribia mwisho wa makala hii naona sina budi kuwaasa wanawake kuwa kwa kiwango kikubwa wanaume wa kisasa walio wa kweli wamebadilisha hisia zao kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii. Vilevile wapo walio katika hatua mbalimbali za kuekea kwenye mageuzi yanayotarajiwa.

Tuendelee kutembelea blog yetu LOVE CLINIC
Kwa mawasiliano Zaidi kama una changamoto yeyote, matukio, habari, elimu na ushauri usisite kuwasiliana nasi:

Whatsapp: +255745222780

Share on Google Plus

About Mlaki

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment