Bila shaka baada ya kusoma mada hii utawenza kuwa na mwanga
juu ya msongo/stress na unaweza kujigundua au kumgundua mtu wako wa jirani
anayesumbuliwa na msongo hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuondokana na tatizo
hili.
Zifuatazo ni mbinu ambazo zitakusaidia namna ya kujitibu
mwenyewe na kumaliza kabisa tatizo la msongo wa mawazo au Stress
-Baada ya kugundua kuwa umesongeka, kaa chini tuliza akili
yako na jiulize ni kitu gani unachodhani ndicho kilichosababisha ukawa katika
hali hiyo.
-Badili namna unavyofikiri. Badala ya kufikiria kushindwa,
kukata tama na kupoteza matumaini maishani mwako, jiambie kuwa unaweza
kufanikiwa na una uhakika wa kufika pale unapopataka.
-Acha kuhesabu mabaya yaliyokutokea hata kama ni mengi na
makubwa kiasi gani na badala yake utazame upande mzuri wa maisha yako hata kama
kuna mambo machache na madogo uliyoyafanya vizuri. Endelea kufikiri vizuri kwa
kadiri uwezavyo. Tazama upya na rudia kujifunza namna ya kufikiri vizuri.
-Usiruhusu mwili wako ukakaa bila shughuli yoyote. Fanya kazi
za mikono kadiri uwezavyo, fanya mazoezi na shiriki kwenye michezo unayoipenda
zaidi. Utafiti umeonesha kuwa mazoezi ya mwili yana umuhimu mkubwa sana wa kupunguza
au kumaliza kabisa tatizo la msongo.
– Fanya mazoezi ya kupumua vizuri na kupumzisha mawazo yako.
Kupumua kwa kuvuta pumzi ndefu puani taratibu na kuitoa kupitia mdomoni
kunaelezwa kuwa husaidia sana kutuliza mawazo.
-Sali kila siku kwa imani ya dini yako. Inaelezwa kuwa sala
hasa zile za usiku husaidia sana kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la msongo.
Tahajudi (Meditations) nayo husaidia kwa kiwango kikubwa sana kumaliza msongo.
-Fanya yale mambo ambayo huwa unayafurahia sana maishani
mwako. Jilazimishe kufurahi hata kama bado unajihisi kuelemewa na huzuni. Kwa
kufanya mambo yanayotufurahisha , tunakuwa tunalazimisha akili zetu kuingiza
kitu kipya, furaha, ambayo huchukua nafasi ya hisia chungu zilizotuletea msongo
wa mawazo/Stress.


HUTAKIWI KURUHUSU MSONGO WA MAWAZO KUKAA MUDA MREFU KICHWANI
MWAKO
-Matumizi ya vidonge kwa ajili ya kuondoa msongo yanapaswa
kuzuiwa kwani hutoa nafuu ya muda mfupi na baada ya nguvu ya dawa kuisha
mwilini, tatizo huwa kubwa mara dufu.
-Jenga mazoea ya kutembelea sehemu zenye mandhari tulivu
yatakayokufanya ufarijike na kujisikia amani ya nafsi. Tembelea sehemu kama
fukwe za bahari, bustani nzuri za maua au sehemu nyingine tulivu.
-Kaa sehemu yenye utulivu au kukaa na rafiki unaemwamini
ongeleeni maswala ya yanayofurahisha na kuleta faraja katika maisha, mapenzi,
muziki, kusikiliza nyimbo za taratibu au hata nyimbo za Dini.
Tunawapenda sana wadau wetu wa LOVE CLINIC tunawaomba sana
muwe karibu nasi na tutaendelea kuwaletea mada nzito nzito na tamu kwa
kuelemishana na kupeana changamoto kwa nia ya kutoana ukungu ulio ndani yetu.
Tuwasiliane kwa email mossesshio@gmail.com
au namba ya whatsapp 0745222780 kama una lolote katika kuboresha blog yetu.
Karibuni sana
0 comments :
Post a Comment