Kwa mwanamke kuchelewa kupata hedhi huwa hakushitui endapo
mwanamke atakua anajua ni nini tatizo au sababu iliyopelekea yeye kukosa hedhi.
Na majibu ya kuchelewa kwa hedhi hupatikana pindi hedhi hiyo inapochelewa.
Mfano kama ulikua unategemea kupata mimba, ikichelewa inakua ni dalili ya
kwanza ya wewe kuanza kufikiria jambo ulilolitaka ninaelekea kutimia na hata
ukatabasamu na kuwaza hatua nyingine ya kujipima nyumbani au kuenda hospitali.
Na kama hukuwa umetarajia ndio hivyo tena mawazo ya kila aina yatakuja kichwa
kutaka kujua kwanini hedhi yako imechelewa na pengine usipate majibu kabisa.
Kwa uchache hapa nimekuwekea sababu 6 zinazoweza kusababisha
hedhi ya mwanamke kuchelewa, na nimefanya hivi kwa kutambua kwamba wanawake
wengi hufikiria sababu moja tu endapo hedhi yao itakua imechelewa.
1. Mimba
Hii ndio sababu ya kwanza kuja kichwani endapo siku za hedhi
za mwanamke zitakua zimechelewa. Na inawezekana ukawa sahihi!! Na hii hutokea hata kama mwanamke
alishapata dalili zote za kwamba siku zake za hedhi ziko njiani, ila siku
uliyotarajiwa ishuke inakua haishuki. Mara nyingi huwa tunashindwa kabisa
kujizuia kufikiria neno MIMBA!!
Hata kama mtu anafahamu kabisa hakucheza rafu mwezi huo. Kwa ushauri tu ili usipatwe
na msongo wa mawazo zaidi tafuta kipimo binafsi au kama ni ngumu pitia
hospitali upate vipimo.
2. Msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo huleta madhara katika mwili wa binadamu mara
nyingi sana, mfano kuumwa kichwa, kuongezeka uzito, kuota vipele na hata
vidonda vya tumbo, na kama nilivyosema awali , kama tayari umeshajua kwamba
hedhi imechelewa msongo wa mawazo unaoupata kwa kufikiri sababu
ni mimba ikiwa haukuwa umeitarajia unaweza kufanya mwili usiwe katika hali yake
ya kawaida tena na hivyo kuendelea kusababisha kuchelewa kwa siku za hedhi zaidi
na zaidi. Kwenye mwili wa mwanadamu kuna homoni mbili ziitwazo ‘adrenaline na
cortisol’.
Hizi hufanya maamuzi kwenye mwili ya kipi kinaumuhimu zaidi
ya kingine mpaka msongo wa mawazo utakapokuisha. Mara nyingi homini hizi huamua
kuanza kazi katika vitu kama msukumo wa damu na gesi mapafuni, huku kazi
nyingine kama mmeng’enyo wa chakula na mfumo wa kizazi kufuatia baadae na hivyo
hata hedhi itachelewa kushuka kama tatizo ndio hilo.
3. Ugonjwa
Ugonjwa wowote unaweza sababisha hedhi kuchelewa kwa hedhi,
hata kama ni mafua au malaria. Ugonjwa uliona kwa wakati huo utakua ni
kipaumbele cha kila homini mwilini mwako kuundoa kama nilivyoelezea hapo juu
kwa homoni zako kutoa kipaumbele kwa mifumo muhimu zaidi ya kizazi kwa wakati
huo.
4. Kubadilisha mazingira.
Kubadili mazingira kwa hapa naamaani chochote kile ulichokua
unafanya zamani, ukakicha gha􀃗a mfano ulikua unaishi sehemu ya baridi ukahamia yenye
joto na kinyume chake, au kusa􀃖ri muda mrefu, kama ulikua unafanya kazi usiku tu ukaanza
kufanya kazi mchana mara nyingi hii husababisha kukosa au kuchelewa kwa hedhi.
Usihofu endapo unajua ulifanya nini mwezi huo.
5. Kunyonyesha
Kama unanyonyesha hautaona hedhi kwa muda mrefu, japo
hutofautiana kutokana na maumbile ya kila mwanamke kwa sababu prolactin (Homoni inayowezesha uzalishaji
wa maziwa ya mama) huharibu kupevuka kwa yai (ovulation). Wamama wengi hua
hawapati hedhi kwa miezi pale wanapokua wananyonyesha. Lakini kumbuka, kukosa
hedhi haimaanishi kwamba hauwezi kushika mimba, kwa sababu ovulation hutokea
kabla haujapata hedhi yako, inawezekana yai likapevuka na baadae ukapata mimba
kabla hata haujapata hedhi. Kwahiyo ukiwa unanyonyesha hakikisha unatumia
kinga.
6. Madawa
Ukweli ni kwamba kuna dawa maarufu za kusababisha kuchelewa
kupata hedhi. Hizi ni kwa matumizi ya uzazi wa mpango. Dawa hizi huzuia
ovulation kwahiyo kama hakuna ovulation basi hakuna hedhi. Na hizi unaweza fahamu
kama unazitumia kwa hiyo hedhi ikichelewa unakuwa huna wasiwasi, na kama
hufahamu basi endapo utaongea na daktari anayekupangia dawa za uzazi wa mpango
kumbuka kumuuliza madhara yanayotokana na matumizi ya dawa hizo (side effects)
atakazokupa.
0 comments :
Post a Comment