
Helloooo Wadau
wa Love Clinic,
Kutokana na
changamoto iliotuzunguka hasa katika swala la wanaume siku hizi japo kweli kuna
tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haswa kwa mazingira ya mijini, Lakini hili
tatizo linaonekana kukuzwa kuliko lilivyo hadi imepelekea woga mkubwa kwa
baadhi ya wengi wetu.
Ndipo baada
ya kusoma majarida na habari tofauti tofauti katika mitandao nikaona niwaletee
hapa kwenye huu ukurasa na tuweze kufundishana na kuelekezana jinsi ya
kujikwamua na janga hili. kwa machache tu kwa ufahamu mchache nilio nao, Ili niwaalike
wengi wenu kwa msaada zaidi wa mawazo kwa ndugu zetu wanaokutana na mfadhaiko
huu. Nikiamini pia wengi wenu mna utaalamu na mnaoweza kuchambua haya madhaifu
kwa ufanisi zaidi mkatusaidia sana kwenye ubuyu huu.
Yafaa sasa
tujikite kwenye ufumbuzi kuliko kuripoti tatizo na kulaumu. Kadiri
tunavyoendekeza kuripoti tatizo tunawaathiri hata wale waliokuwa wazima ambao
kwa kuwa hakuna kipimo sawia kujua kipi ni kipi, nao wasiwasi unawafanya
wanapoteza ujasiri wao na kujiona wana tatizo kumbe wapo imara sana kuliko
mkuki.
Kwa kuanzia
yafuatayo yaweza kusaidia kuboresha kulifurahia tendo la ndoa zaidi na kwa muda
zaidi.
Kuuweka Mwili vizuri: Ni wazi kuwa tendo hili linachagiwa
sana na mzunguko mzuri wa damu. Mwili ukiwa kwenye hali nzuri kiafya na tendo
huwa linaenda ipasavyo. Na mwili ukiwa dhoofu basi tegemea tukio dhoofu pia.
Hivyo ukitaka kuwa na matokeo mazuri kwenye ndoa yako, jitahidi sana kujiweka
vizuri kwa kula sahihi na kufanya mazoezi mepesi mepesi tu kwa wale wanaoweza
kuutumia muda vizuri wapiti pite Gym walau siku mbili na kuendelea kwa wiki.
Kufahamu
kuwa kupumzika kwa uume baada ya kufika mara ya kwanza sio tatizo. Kwa wanaume
walio wengi, baada ya mshindo wa kwanza hupumzika kidogo kabla ya kuendelea na
awamu nyingine. Japo kuna ambao wana uwezo wa kuendelea moja kwa moja bila
kupumzika (law of use and misuse inahusika kwa wengine apa). Kwa hio kusinyaa
kwa uume baada ya mshindo wa kwanza, isifahamike kuwa ni upungufu wa nguvu bali
ni ajdustiment ya mwili wenyewe kutokana na kwamba mwanaume kabla ya tendo
mapigo ya moyo huongezeka na huchangia damu kwenda kwa kasi, na kwa hali hio
anakua yupo juu sana kimhemko, inapofikia anamaliza raundi ya kwanza mwili
unakua unapoa /umesharudi kwenye hali yake ya kawaida, ndiko kunakosababisha
hio maneno ya kusinyaa, kwa wengi wakati mapigo ya moyo yanaporudi kawaida
(MWILI KUPOA).
Maandalizi
ya mwili. Wanaume tupo tayari muda wote ila linapokua swala la mwenza wako (kwa
kuwa muda unaotumia kwa maandalizi na tendo una uhusiano wa moja kwa moja na
satisfaction ya mwenzio unahitaji muda angalau nusu saa na kuzidi kujiandaa na
mwenzi wako. Kama timu ya mpira inapoenda ugenini huhitaji muda kuzoea
mazingira, ndio na mwanaume anavyohitaji muda kuzoea mazingira ya ugenini. Hili
linakusaidia sana mwanaume kutoka kwenye mihemko na kurudi kwenye hali yako ya
kawaida ambayo itakusaidia kuwa na muda mzuri zaidi wa kufurahia tendo.
Jitahidi pia kuvuta pumzi nyingi ndani na uiachie polepole kukusaidia kukuweka
kwenye utulivu mzuri.
Timing ya kuanza tendo: Kwa kuwa tendo linahusisha sana
hisia za mwili, ukiwa umetumia muda unaotosha kuandaana, basi usiwe na papara
mwanzoni, bali uwe na utulivu, pia jitahidi kuzungumza moja mawili wakati
unaanza kuzoea mazingira mengine (core business) EPUKA UHARAKA na kuweka sana
akili yako hapo, jinafikie mwenyewe kuwa it’s just a normal thing (mental
pride)
Concetration/
Umakini uliopitiliza Unapaswa kumfanya mkeo aweke akili yake yote hapo, na wewe
unatakiwa katika kumuweka mkeo kwenye concentration uuharibu umakini wako
(level of concentration). Ukiweka concentration ya juu sana kwenye tendo
haikuchukui dakika mbili umemaliza, na kuirudisha tena ile hali ya
concentration uliokua nayo mwanzo itakuwia ngumu sana.. Usiweke sana akili yako
hapo kama unataka kufurahia kwa muda zaidi. ila kama hutaki kudumu.. weka akili
na umahini wako hapo woote.. just seconds or a minute you are done
MAZOEZI ya
mwili ni muhimu sana sana sana sana sana kwetu wanaume. Kama huna muda wa
kwenda jimu walau ukiamka piga PUSH-UPS walau 50'' kila siku na ''SQUARTS'' .
haya ni mazoezi mepesi lakini ni BORA zaidi kwa mwanaume. Kwetu sisi wanaume
tunatumia sana misuli yetu wakati huu, kwa hio kuna ulazima wa kutafuta
ustahimilivu wa misuli ''mussle strength n perseverance''. Hio kitu ni starehe
na unatakiwa baada ya tendo uwe umekuwa refreshed na sio uwe unaumwa kila
mahali na sijui joints zinauma sijui nini nini? ukijiona unakuwa hivyo baada ya
tendo ujue mwili wako haujakaa fiti ipasavyo kimazoezi/kiafya
Pia Afya ya
Akili inahusika sana, Japo inahitaji jitihada makhususi... lakini kila mtu ana
uwezo wa kuchagua nini cha kufikiria na nini si cha fikiria(kupuuzia) na pia
akienda hatua zaidi anaweza kupuuza kila kitu kwa wakati fulani kama unajua una
huo uwezo na ukaamua kuutumia. Pia kuchagua kufikiri yale yaliopo kwenye uwezo
na urefu wa kamba yako pekee; vitu usivyo na uwezo navyo utajisumbua tu bure na
kujipa stress zaidi. Weka nguvu na jitihada zako kwenye kutafuta ufumbuzi wa
changamoto zako, jifunze na acha kufikiria matatizo kwa maana hakubadilishi
kitu na yataendelea kuwa hivyo n.k n.k................ Ukiwa na namna nzuri ya
kuyachanganua mambo yako utasaidika sana kwenye afya ya akili yako na kuwa
vizuri zaidi
Karibuni
wadau kusaidia utatuzi wa hili jinamizi linalojizolea umaarufu kadiri siku
zinavyokwenda kwenye jamii yetu.
0 comments :
Post a Comment