Kumekua na
malalamiko kila kona kwamba wapenzi wao wanawasaliti na kujikuta wanaingia
katika maumivu na mateso yanayowafanya kulia kila iitwayo leo jambo ambalo
limenifanya leo nikuletee mjadala huu. Je UNAFANYA YAPI KUZUIA MPENZI WAKO
ASIKUSALITI?
Ni kweli
mapenzi ni imani, yaani kuamini kwamba uliyenaye anakupenda hata kama ukweli
unaweza usiwe hivyo. Wengi walio na wapenzi wanajiaminisha kwamba
wanavyowapenda wenza wao ndivyo wanavyopendwa.
Pia wapo
ambao wanaamini kwamba eti kwa namna wanavyoonesha mapenzi yao, hata kwa dawa
hawawezi kusalitiwa. Utamsikia mwanamke akisema; “bwana wangu mimi kwangu
hapindui, ananipenda sana na hawezi kunisaliti”.
Mtu
anayesema maneno hayo anajipa imani na ukifuatilia unaweza kukuta huyo
anayesema hivyo, mpenzi wake ni kiwembe ile mbaya.
Ni wanaume
wangapi ambao wewe unawajua wake zao wanawaamini sana lakini kumbe wanasalitiwa
sana kwa siri? Ni wanaume wangapi, tena wengine wakiwa marafiki zako ambao
wake/wapenzi wao wanawaamini sana lakini wanasifika kwa kupenda totozi?
Watu hao
wako huko mtaani, tena wengi tu na yawezekana hata mpenzi wako unayemuamini
sana si muaminifu, anajifanya ni mtu mpole, anayejiheshimu, asiye na mawazo ya
kukusaliti lakini kumbe akiwa mbali na wewe, ni hatari.
Lakini sasa,
kama ukweli uko hivyo, tuna sababu ya kuishi kwa hofu tukihisi kwamba wapenzi
wetu si waaminifu? Hapana! Kuishi kwa wasiwasi ni kujipa presha za bure na za
kujitakia.
Ni kweli kwa
ulimwengu wa sasa hakuna mtu ambaye anaweza kumuamini mpenzi wake kwa asilimia
zote lakini kisaikolojia unatakiwa kumuamini kwa asilimia zote huyo uliyenaye.
Hata kama
yapo anayofanya akiwa mbali na upeo wa macho yako, iwe ni yeye na Mungu wake
lakini kwa kuwa hujawahi kumfumania wala kuona ishara zozote za kwamba
anakusaliti, jenga imani naye.


Imani
unayojipa ni kwa lengo la kujipa amani ya moyo, uishi kwa furaha na kujiweka
mbali na presha zisizokuwa na msingi.
Ila sasa,
nawashangaa sana wale ambao wanajiaminisha kwamba wapenzi wao hawawezi
kuwasaliti kwa namna yoyote. Unajua kwa nini nawashangaa?
Ni kwa
sababu huko mtaani kuna vishawishi vingi sana, wapo wasichana wazuri sana ambao
wao hawajali kwamba huyu ni mume wa mtu, watamtega kwa kila namna ili wamnase.
Wapo
‘ma-handsome’ na mapedeshee ambao wakimtaka mwanamke yeyote watafanya kila njia
wampate. Sasa wewe ambaye uko kwenye uhusiano unafanya yapi ya kumfanya mwenza
wako ayashinde majaribu?
Maana usikae
na kusema mpenzi wako hakusaliti, lazima uwe na sababu za kusema na
kujiaminisha hivyo. Je, umejenga mazingira ya mpenzi wako kukuona wewe ndiyo
wewe wengine takataka? Kama hujafanya hivyo usijidanganye, kaa ukijua wajanja
wanakumegea penzi lako.
Ninachotaka
ukijue leo kupitia makala haya ni kwamba, huko mtaani kuna mitego mingi kwa
wapenzi kiasi kwamba ni wachache sana wanaoweza kuikwepa. Mfanye mpenzi wako
awe kati ya wale ambao hawanasiki kirahisi.
Mpende,
mjali, mthamini, mpe penzi linalostahili lakini pia zungumza naye kila mara
kwamba, hao wazuri huko nje wanaomtaka, hawana mapenzi ya kweli. Ni walaghai tu
wanaomtamani ila mwenye mapenzi ya kweli kwake ni wewe.
Pia zungumza
naye kuhusu magonjwa, mueleze kabisa kwamba, hata kama kwa tamaa zake
atakusaliti huko gizani, magonjwa yatakuja kumuumbua.
Naamini
ukifanya hivyo, hata kama hutawaambia watu kwamba mpenzi wako hawezi kukusaliti,
wewe mwenyewe utakuwa na imani kubwa kwa kuwa umemuandaa kukwepa vishawishi.
Tujadiliane kwa
mapana hapa ili kupeana changamoto za kina kujua nini cha kufanya kuweza
kulinda mahusiano yetu ili kuondoa michepuko na kusalitiwa. Nini tufanye kuzuia
wapenzi wetu au kutosalitiana????
Kwa
matukio/changamoto/shuhuda/mada na jambo lolote linalohusiana na LOVE CLINIC wasiliana nasi:
Barua pepe: mossesshio@gmail.com
Whatsapp No:
0745222780
0 comments :
Post a Comment