
Hivi huu ni ulimbukeni wa mavazi au ni kuiga tabia zisizo na
kichwa wala miguu???
Tabia za wadada wengi hasa wa mijini
Baadhi ya Wadada wa Darisalamu shida kweli, sasa nguo fupi
umevaa mwenyewe ya nini kuhangaika kushusha shusha chini unavotembea. Wenzenu
hizo wanavaaga wakiwa na magari yao wakielekea maeneo ya hadhi zao, sasa wewe
nawe na kinguo chako kifupi unapanda basi la mwendokasi kuelekea Karume kununua
mitumba huku ukikazana kuvuta chini kisketi chako kifupi, kwani ulivalishwa?
Kama umeamua kuwafaidisha watu waache wafaidi, kwanini
msivae nguo zenye heshima na kuwastiri miili yen utu usiangaike kuvuta chini.
Hizo akili sijui hua mnafungiaga kwenye kabati mkiondoka makwenu? mnavuruga
akili na swaumu za watu mjue. vaa nguo ambayo utakua comfortable nayo!!!
Wanawake wengi mpaka mnakua mnajidhalilisha wenyewe halafu
mkiambiwa mnaona kama mmekosewa hebu jiheshimuni jamani kwa wakati huu sio wa
kati wa kuoneshana vichupi au mapaja yenu. Muwe na siku njema
Wewe mwanadasa unaejitambua hebu ungana na Love Clinic
kukemea hali hii ya wadada wenzio sisi wanume tumechokaaa!!!!!!
0 comments :
Post a Comment