Mara nyingi
asilimia kubwa ya wanawake hupenda kuwa na wanaume wanaojiweza kiuchumi. Lakini
baadae wanapotambua kwamba mwanaume huyo ameshaoa hushangaa sana, huumia na
kusema waliwaamini kuwa wako single na kwamba wanaume wote ni mbwa tu.
Wanaume sio
mbwa au paka shume, ni nyie wenyewe ndio mnashindwa kuwaelewa na hamtaki
kufanya uchunguzi. Mlishaambiwa kwamba nyuma ya mwanaume mwenye MALI na
MAFANIKIO kuna mwanamke. Na wewe unataka mwanaume aliyefanikiwa. Unategemea
nini?
Kama
utakutana na mwanaume ambae ni handsome, ana mali, anaendesha gari nzuri, yuko
vizuri kiuchumi, basi huyo sio mumeo mtarajiwa, huyo ni mume wa mtu fulani kwa
muda huo. Ni agharabu sana kukutana na mwanaume anayejiweza halafu akawa
single, either uwe shareholder au unyang'anye share zote za mwanamke mwenzako
kitu ambacho sio busara hata kidogo.
Mume wako
mtarajiwa yupo anahangaika kutoka na maisha, anapigania ndoto zake. Huenda yupo
shambani, yupo dukani, anapiga kitabu chuo, au yupo anabeti. Kimsingi yupo
anapigania kuchomoka kimaisha. Anakusubiri tu wewe umpe support na back up ya
kutosha.
hebu
tushauriane hapa wewe na love clinic nini kifanyike na tuweze kujitoa katika ulmwengu
huu wa maumivu ya kila siku hasa kwa wadada
0 comments :
Post a Comment